Hatimaye Uongozi wa Azam FC umethibitisha taarifa za kukubaliwa kuutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam watakapocheza dhidi ya Young Africans.

Azam FC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Jumapili (Machi 17), ambao awali ulipangwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika kurasa za Mitandao ya Kijamii za Azam FC imeeleza kuwa mchezo huo utaanza saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

May be a graphic of 1 person, playing American football, playing football and text

“#VenueChanged Mchezo wetu ujao wa Ligi Kuu ya NBC, dhidi ya Yanga, sasa utafanyika Uwanja wa Mkapa badala ya ule wa Azam Complex uliopangwa hapo awali.”

“Mchezo huo unatarajia kufanyika Jumapili hii, saa 1.00 usiku.”

Ikumbukwe kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umefungwa kwa muda, ili kupisha maboresho yanayoendelea kufanywa uwanjani hapo kwa ajili ya Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN 2024’ zitakazoandaliwa na Tanzania, Kenya na Uganda.

Uwanja huo ulipangwa kutumiwa kwa ajili ya Michezo ya Simba SC dhidi ya Young Africans pamoja na Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Vitita vya Mafao: NHIF, APHFTA warudi mezani
Julio anasubiri muda Singida FG