Mlinda Lango wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, Ederson huenda akaukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal utakaopigwa Machi 31.

Mlinda Lango huyo anahofiwa kuukosa mchezo huo ambao huenda ukawa sehemu ya maamuzi ya Ubingwa msimu huu, anasumbuliwa na jeraha la misuli, ambalo huenda likamuweka nje kwa muda wa majuma manne.

Mlinda Lango huyo kutoka nchini Brazil aliumia alipomchezea vibaya Darwin Nunez wakati City ikitoka sare ya 1-1 dhdii ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield, Ederson akisababisha Penati ambayo ilipigwa na Alexis MacAllister na kuisawazishia The Reds.

Ederson pia anatazwamiwa kukosekana kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Newcastle United  ambao utapigwa kabla ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa.

Kwa mujibu wa BBC Sport, Man City wameifahamisha Brazil kwamba, Ederson hatakuwa fiti kwa michezo hiyo ya kimataifa, ambapo Selecao wanatarajiwa kumenyana na England na Hispania katika muda wa siku tatu.

Baada ya kurejea kwa Premier League, Man City itawakaribisha Aston Villa mnamo Aprili 3, kabla ya kusafiri kusini mwa London kumenyana na Crystal Palace ya Oliver Glasner mnamo Aprili 6.

Kamati ya Bunge yakagua ujenzi Jengo la Wizara ya Nishati
Mama aliyeuwa Wanawe kwa Sumu Mbeya naye afariki