Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Angel Gamondi, amesema haipendezi kwa baadhi ya Mashabiki kuiondoa timu yake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, baada ya kupangwa kwa Droo ya Robo Fainali.

Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ jana Jumanne (Machi 12) ilipanga Droo ya Robo Fainali, huku Young Africans ikipangwa na Mabingwa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundown.

Gamondi amesema Young Africans ina nafasi ya kutinga Nusu Fainali kama ilivyo kwa Sundown, hivyo kikosi chake kinapaswa kupewa heshima na sio kubezwa.

Amesema huenda wapinzani wao wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutoka na muonekano wa kiuchumi, lakini kwake anaamini soka halina tabia ya kuangalia nani ana kiasi kikubwa cha pesa, zaidi ya kuziacha dakika 90 ziamue.

“Hakika ikiwa utalinganisha bajeti ya Sundowns na yetu, bila shaka wao lazima uwape nafasi kubwa ya kushinda. Mara ya mwisho walimnunua mchezaji mmoja kutoka Argentina kwa dola milioni 4 na sisi tukamleta Guede na Okrah bila gharama yoyote (free agent). Hii ndio tofauti, lakini hiyo haina maana wakati mwamuzi anapopuliza filimbi ni 11 dhidi ya 11.” Amesema Gamondi

Wakati Young Africans ikipangwa na Mamelodi Sundown, watani zao Simba SC wamepangwa kukutana na Mabingwa watetezi wa Barani Afrika Al Alhly ya Misri.

Michezo mingine ya Robo Fainali, TP Mazembe ya DR Congo imepangwa kukutana na Mabingwa wa Soka nchini Angola Petro De Luanda, huku Esperance Tunis ya Tunisia itapapatuana na Mabingwa wa Soka wa Ivory Coast Asec Mimosas.

Julio Kocha Mkuu Singida Fountain Gate
Wenye nia njema, ovu watembelee Makaburi ya Kimbari