Familia za Kitongoji cha Kuzuia A, zilizopo Kata ya Kiroka, Tarafa ya Mkuyuni, Wilaya ya Morogoro Vijijini, zimeunganishwa na Polisi Kata kwa lengo la kushirikiana kwa pamoja kwenye mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

Akizungumza na familia hizo, Polisi Kata wa Kata hiyo Mkaguzi wa Polisi, Dhikiri Pori amesema ilikuwa ni kawaida kwa jirani kumuona mtoto wa mwenzie akifanyiwa ukatili na kukaa kimya kwa sababu sio sehemu ya familia yake au anaogopa kusema ili asionekane mbaya dhidi jirani yake.

Amesema, jambo hilo linatakiwa kukemewa vikali na kuwataka wawaone watoto wote kama ni wao na waumizwe na kuguswa kwa kufanyiwa kwao ukatili, huku akitoa namba za simu ili kupenyeza taarifa za siri kwa Polisi Kata kama kutakuwa na hofu.

“Muunganiko huu utawasaidia Ulinzi kwa watoto wenu hata kama baadhi yenu hamtakuwepo nyumbani wakati matukio yanatokea. Kitendo cha kuoneana muhari kwenye matukio ya Ukatili ni hatari na hatari zaidi ni pale mnapoyamaliza kifamilia bila kuhusisha vyombo vya Dola.” amesema Pori

Aidha, aliwafundisha mambo kadhaa yakiwemo ulinzi jirani, usalama wao kwanza, familia yangu haina muhalifu na utii wa sheria bila shuruti.

Ahukumiwa kifo kwa mauaji ya Monica
Minada ya Vito Tanzania yawavuta Wazimbabwe