Klabu ya Manchester United inataka zaidi ya Pauni 43 milioni kwa ajili ya kumuuza Mshambuliaji wao, Mason Greenwood, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyo wa kimataifa wa England ambaye kwa sasa anaichezea Getafe, msimu huu ameonyesha kiwango bora kiasi cha kuvutia vigogo mbalimbali Barani Ulaya ikiwamo Barcelona.

Hivi karibuni mabosi wa Man United, John Murtough na Matt Hargreaves walionekana jijini Barcelona, Hispania na walikuwa kwenye kikao na mkurugenzi wa masuala ya michezo wa Barcelona, Deco na baadhi ya vigogo wengine ikiwemo wakala Federico Massai.

Kikao hicho kinadaiwa, kilikuwa na mpango wa kujadili uwezekano wa Greenwood mwenye umri wa miaka 22 kutua Barca mwisho wa msimu huu, imeripoti tovuti ya Manchester Evening.

Ukiiondoa Barca, kuna timu kutoka Saudi Arabia zilizoonyesha nia ya kumsajili ingawa inaonekana kuwa ngumu kujiunga nazo kwa sababu bado anahitaji kuendelea kucheza soka la kiushindani Barani Ulaya kwa msimu ujao.

Greenwood alitua Getafe dirisha lililopita la majira ya kiangazi, baada kukaa nje ya uwanja tangu Januari 2022, aliposimamishwa kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia zilizokuwa zinamkabili.

Singida FG wafichua mkataba wa Julio
Kizungumkuti mgomo wa Madaktari ukianza rasmi Kenya