Maboisi wa Manchester City wamesitisha mazungumzo na wawakilishi wa kiungo Kevin de Bruyne yaliyokuwa na lengo la kumsainisha mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Mazungumzo hayo yamesitishwa kwa kile kinachoelezwa wanaweka umakini zaidi kwenye mechi za timu hiyo katika michuano mbalimbali.
De Bruyne mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2025, na hivi karibuni Man City ilidaiwa kuwa tayari kumuuza ikipata ofa nono.
Mara kadhaa matajiri kutoka Saudi Arabia wameonyesha nia ya kumsajili nyota huyu na kuwa tayari kutoa zaidi ya Pauni 100 milioni kama ada ya uhamisho na kumpa mshahara mara tatu ya ule anaoupokea Man City kwa sasa.
Hata hivyo, baada ya kusambaa kwa taarifa hizo, Man City iliingia naye mazungumzo ili asaini mkataba wa kuendelea kuitumikia kwani kocha Pep Guardiola bado anahitaji huduma yake.