Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, kupitia misako mbalimbali limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 21 waliokuwa na Dawa zza kulevya aina ya Mirungi Kg 549.8, 14 wakiwa na Bangi Kg 157.5 pamoja Pikipiki 7 zilizokuwa zikitumika katika uhalifu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari hii leo Machi 18, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Justine Masejo amesema mafanikio hayo yametokana na operesheni mbalimbali zilizofanywa na jeshi hilo dhidi ya uhalifu na wahalifu.

Amesema, watuhumiwa wengine wawili walikamatwa wakiwa na vipande viwili vya Pembe za Ndovu na wote wamefikishwa Mahakamani na kuhukumiwa kwenda Jela kifungo cha miaka 20 kila mmoja.

Kamanda Masejo amesema, pia walifanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 25 wakiwa na Pombe ya Moshi lita 143 na watuhumiwa wote wamefikishwa Mahakamani kwa taratibu za kisheria, huku wengine 19 wakikamatwa kwa makosa ya ulawiti na ubakaji, ambapo mtuhumiwa mmoja kati ya hao amehukumiwa kifungo cha Maisha Jela kwa kosa la ulawiti.

Kesi ya Gekul: Ngoma bado mbichi Manyara
Maganya: Wizara iache urasimu kwenye ujenzi wa Vyuo