Aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Paulo Teveli amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela bila faini, baada ya kutiwa hatiani kwa uhujumu uchumi.
Teveli alikuwa akikabiliwa na makosa mawili, ikiwemo matumizi mabaya ya mamlaka chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 na kosa la ufujaji na ubadhirifu wa shilingi 8,377,000.
Fedha hizo zilikuwa ni za makusanyo ya kila siku kutoka kwa Wagonjwa ambazo hakuzipeleka benki katika kipindi cha mwaka 2020, ambapo mbali na adhabu ya kifungo hicho, pia Taveli ametakiwa kurejesha fedha alizofanyia ubadhirifu.