Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imezialika kampuni zote za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi kushiriki katika Duru ya kwanza.

Dkt. Mwinyi amesema hayo hii leo Machi 20, 2024 wakati akizindua Duru ya kwanza ya Utoaji wa vitalu kwa Kampuni za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia maeneo ya baharini Zanzibar.

Amewakikishia wawekezaji wote wa sekta ya mafuta na gesi kuwa Serikali iko tayari kuwahikikishia mazingira mazuri ya uwekezaji kwa manufaa ya wote.

Aidha, Dkt.Mwinyi pia ameeleza dhamira ya Serikali katika uchumi wa buluu kuwa ni kuimarisha uchumi wa nchi kwa haraka na kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo endelevu ya vyanzo vya nishati ya uhakika.

Nunez ajiondoa Uruguay
Ihefu FC yahamia jijini Arusha