Leo ni Siku ya Kimataifa ya Furaha, ambapo kwa mara ya saba mfululizo nchi ya Finland imetangazwa kuwa raia wake wana furaha zaidi duniani, ikifuatiwa na majirani zake wa eneo la Nordic, ambao ni Sweden, Denmark na Iceland.

Kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka inayotolewa na Umoja wa Mataifa, imearifu kuwa imebaini kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na furaha hasa miongoni mwa Vijana katika Mataifa ya Magharibi.

Mataifa ya Ujerumani na Marekani yameondolewa katika orodha ya nchi 20 bora zenye furaha duniani na nafasi zao kuchukuliwa na Nchi za Costa Rica na Kuwait ambapo nchi za Ulaya Mashariki za Serbia, Bulgaria na Latvia zenyewe zina ongezeko kubwa la furaha.

Nafasi ya mwisho katika orodha hiyo inashikiliwa na Taifa la Afghanistan ambalo limekumbwa na janga la kibinaadamu na hivyo raia wake kuwa miongoni mwa wale wasio na furaha kabisa.

Uhuru wa Mwandishi Bujakera: Tshisekedi atajwa
Nunez ajiondoa Uruguay