Mawakili na baadhi ya marafiki wamethibitisha kuachiwa huru kwa Mwanahabari mashuhuri wa DRC, Stanis Bujakera aliyekuwa kizuizini kwa zaidi ya miezi sita.

Machi 18, 2024 Bujakera (33), alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela akidaiwa kuandika Makala iliyotuhumu idara ya ujasusi ya Jeshi kuhusika na mauaji ya Mwanasiasa wa upinzani, Cherubin Okende.

Taarifa anayodaiwa kuandika, ilichapishwa katika jarida la Jeune Afrique na ilinukuu vyanzo kadhaa vya kijeshi, kabla ya mamlaka kujitokeza kudai kuwa sehemu kubwa ya tarifa zilizoandikwa zilikuwa za kughushi.

Awali, waendesha mashtaka walitaka mwanahabari huyo ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela na huenda kuachiwa kwake kulitokana na shinikizo kutoka Serikalini, baada ya Rais Felix tshisekedi kusema angefuatilia kesi ya Mwanahabari huyo.

Tshabalala aweka matumani kwa Benchikha
Finland yaongoza kwa mara ya saba Nchi yenye furaha Duniani