Kocha wa Ihefu FC, Mecky Maxime, amesema anaendelea kuijenga timu yake baada ya ligi kusimama na kuhakikisha inafanya vizuri, kujinasua katika nafasi za hatari katika msimamo.

Ihefu ipo nafasi ya 11 ikiwa na alama 23 baada ya kushinda mechi sita huku ikitoka sare michezo mitano na kupoteza mechi 11 baada ya kushuka dimbani mara 21, huku ikibakiwa na michezo tisa kabla ya kumaliza ligi.

Mexime amesema kikosi chake kimekuwa na kiwango bora tangu ulipoanza mzunguko wa pili jambo ambalo limesaidia kupata matokeo chanya, kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo.

“Laiti kama ligi isingesimama, naamini timu yangu ingekuwa imepata matokeo mazuri na kuwa juu katika msimamo, hata hivyo nautumia wakati huu kuboresha baadhi ya safu kwa lengo la kutafuta ushindi katika michezo ijayo,” amesema

Kocha huyo ambaye pia ni nyota wa zamani wa timu ya taifa Taifa Stars, amesema bado kikosi chake kinapaswa kupambana kwani nafasi ya 11 bado si nzuri.

Amesema atakuwa na amani kama timu yake itakuwa katika timu 10 bora na kuondokana na presha ya kucheza mechi za mtoano za kuwania kubaki Ligi Kuu.

Ihefu inatarajivwa kurudi dimbani Aprili 13, mwaka huu kupimana ubavu na Simba SC katika mchezo wa mzunguko wa 22.

Masoud Djuma amerudi tena Bongo
PPRA Tanzania, Bangladesh wabadilishana uzoefu matumizi mifumo ya Tehama