FC Barcelona ipo katika nafasi nzuri ya makubaliano ya kumwajiri Kocha wa Sporting CP Ruben Amorim, huku kukiwa na hofu Liverpool huenda ikaongeza nia yao ya kumtaka mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 39, kwa mujibu wa ripoti.

Kocha wa sasa wa Barca, Xavi atajiuzulu wadhifa wake mwishoni mwa msimu huu, na licha ya klabu hiyo kujaribu kumzuia, gwiji huyo wa Camp Nou hivi majuzi alisisitiza hajabadill uamuzi wake.

Kutokana na hali hiyo, Barcelona wanasaka kocha mkuu mpya na kwa mujibu wa gazeti la The Independent, wanalenga kumfuata Amorimn.

Ripoti hiyo inadai Barcelona kwa muda mrefu inaonekana kupendezwa kumpata Amorim huku Liverpool na Bayern Munich, ambao pia wanahitaji makocha wapya kabla ya msimu ujao kuchukua nafasi za Jurgen Klopp na Thomas Tuchel, walikuwa na malengo ya kumchukua, Xabi Alonso wa Bayer Leverkusen.

Hata hivyo, Alonso hivi karibuni alithibitisha uamnuzi wake wa kubakia msimu huu wa joto, mbio za kumwania Amorim zimepulizwa na Barcelona sasa wanasemekana wako mbioni kukamilisha dili hilo kabla ya Liverpool au Bayern kujaribu kumpata.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Makamu wa Rais wa Barcelona, Rafa Yuste, alikiri wazi ataendelea kujaribu kumshawishi Xavi kubaki, akipendekeza kwa sasa hakuna mpango wa kutafuta mrithi kule Katalunya.

“Nitajaribu kumshawishi Xavi, lakini ni uamuzi ni wake kibinafsi,” alisema Yuste.

“Bado kuna michezo ya ligi iliyobakia, Ligi ya Mabingwa Ulaya, inabidi tumwache aifurahie. Natumaini na ninatamani aendelee kwa sababu tunazungumza juu ya mradi wa muda mrefu naye, sio msimu mmoja au miwili.”

Kipengele cha juu cha kutolewa kwa Amorim, kinachoaminika kukaribia pauni milioni 13, kinaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa Barcelona.

Singida Black Stars yaanika malengo yake
DCEA yanasa zaidi ya kilo 54,000 Dawa za kulevya