Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wakala wa misitu – TFS, imefanya operesheni katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Iringa, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata jumla ya Kilogramu 54,506.553 za dawa za kulevya za mashambani na viwandani pamoja na kuteketeza ekari 262 za mashamba ya bangi.

Akiongea na Waandishi wa Habari hii leo jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema Dawa zilizokamatwa ni bangi kilo 54,489.65, mirungi Kilogramu 10.3, heroin gramu 90.93, cocaine gramu 1.98 na Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa methylene dioxy pyrovalerone (MDPV).

Dawa hiyo mpya ilikamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32). Watuhumiwa 72 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.

“Methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) ni dawa mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu. Dawa hii ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Pia, imeongezwa nguvu ya kilevi ya kilevi inayozidi inayozidi cocaine, heroin namethamphetamine,” alisema Kamishna Jenerali Lyimo.

Aidha, ameongeza kuwa dawa hiyo ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao (internet) na husafirishwa kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majina bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy.

Amesema, Mamlaka pia imebaini uwepo mashamba makubwa ya bangi katika hifadhi za misitu ya Ubangu mkoani Shinyanga na Mabatini mkoani Tabora ambapo wahalifu hao wamekata miti katikati ya misitu hiyo na kulima bangi.

Hata hivyo, Kamishna Jenerali Lyimo amesema “kwa ushirikiano tulioupata kutoka kwa wakala wa misitu (TFS) tulifanikiwa kuteketeza mashamba hayo na kuwakamata wahusika.

Ruben Amorim azigonganisha Barca, Liverpool
Hersi: Timu ipo tayari kupambana Afrika Kusini