Licha ya timu yake kuburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema anataka kuona kikosi chake kinatinga hatua ya Nane Bora ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Tanzania BAra (Kombe la CRBD Bank).

Mtibwa Sugar wanajiandaa kuikabili Azam FC katika mchezo wa hatua ya 16 Bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara utakaochezwa Jumapili (Aprili 07) katika dimba la Azam Complex, Dar es salaam.

Katwila amesema wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo licha ya kuwa watafanya ‘maajabu’ katika mechi hiyo, huku akifichua kuyafantia kazi makosa yaliyojitokeza kwenye michezo iliyopita na sasa wako tayari kwa mchezo huo.

Amesema wanatambua ubora wa Azam FC na kwa sababu hiyo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kusonga mbele.

“Katika hatua hii ambayo kila timu iliyopo iko vizuri, ninawaamani vijana wangu watafanya vyema kwa kuyahamisha yale ya mazoezi yuliofanya katika uwanja wa mechi,” alisema kocha huyo.

Ameongeza kuwa wanatakuwa kuongeza umakini kwa sababu watacheza ugenini lakini akiwakumbusha wachezaji wake kutumia kila nafasi itakayopatikana.

Kocha Tanzania Prisons awasubiri KMC FC
Huduma ya Maji: Wananchi walipie wanachotumia - Rais Samia