Lydia Mollel – Morogoro.

Mtu mmoja Ibrahim Juma Ramadhan (44), amefariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa ghorofa lililopo mtaa wa Sugume Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema walifanikiwa kumuokoa mtu mmoja aliyebanwa na ukuta sehemu za miguu yake akiwa hai lakini alifariki baadaye.

Amesema, sababu za ukuta huo kuanguka ni kutokana na jengo lililokuwa linajengwa, kujengwa chini ya kiwango, hali iliyopelekea  sehemu ya ukuta kumeguka na kudondoka, huku akiwataka Wananchi kuchukua tahadhari katika maeneo yote ambayo ujenzi unaendelea.

Aaron Ramsdale kuondoka Arsenal
Benchikha atamba kupindua matokeo Cairo