Kuelekea mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC itakayochezwa April 12, mwaka huu, Benchi la Ufundi la Tanzania Prisons linajipanga kuimarisha safu yake ya ulinzi ili kuhakikisha hawaruhusu nyavu zao kutikiswa.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Hamad Ally amesema makosa machache katika safu hiyo kwenye michezo iliyopita, hivyo anarekebisha mapungufu hayo kwa lengo la kuhakikisha hayajirudii.

“Tunaendelea kujiimarisha kwa lengo la kupata pointi tatu katika mchezo wetu unaofuata, tunajua utakuwa na upinzani mkubwa kutokana na maandalizi yaliyofanywa na pande zote mbili,” amesema Ally.

Ameongeza michezo ya kirafiki waliyoicheza imesaidia kuimarisha miili ya wachezaji wake na anaahidi watapata matokeo chanya na kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kocha huyo amesema afya za wachezaji wake zinaendelea vizuri isipokuwa, Doto Shabani, ambaye ni majeruhi lakini anaamini hali yake itaimarika na kurejea kikosini hivi karibuni.

Bilioni 415 zaweka rekodi Brighton
Zuberi Katwila: Tunaitaka robo fainali shirikisho