Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Maji kuweka utaratibu wa mwananchi kutumia maji kulingana na kiasi alicholipia ili kuondoa malalamiko ya kulimbikiziwa bili za maji.

Rais Samia ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye uapisho Viongozi Wateule katika ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam hii leo Aprili 4, 2024 na kuongeza kuwa Wizara ya Maji na Taasisi husika zinatakiwa kuwasaidia Wananchi, ili waweze kulipia bili ya Maji kwa kile walichotumia.

Amesema, “Bili za Maji ni kilio kingine cha Wananchi, tumelia sana na kubambika bili za Maji tukasukuma Wizara iingie katika Mita, mmekwenda kwenye Mita bado kuna kilio, naomba sana fanyenikama wanavyofanya TANESCO, wekeni mita ya Maji mtu alipe alichokitumia pesa yake ikiihs amita inakata atakwenda kuyanunua mengine.

“Lakini mtu ametumia unakuja kutizama hapa unakwenda kuchungulia unakuta ametumia 40 unamuandikia 80 na bili yako ya nyumbani umemtilia yeye hapana, tafuteni Mita ambazo watalipa jinsi wanavyotumia hilo ndilo agizo langu,” amesema Rais Samia.

Zuberi Katwila: Tunaitaka robo fainali shirikisho
Mikopo: Atakayeunda kikundi hewa amejifukuza kazi - Mchengerwa