Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Rweikiza amewaunga mkono waumini wa dini ya Kiislamu kwa kutoa Sadaka ya Iftar kwenye Misikiti 113 iliyopo jimboni kwake, kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Akikabidhi sadaka hiyo ya Mchele na Sukari kwa katibu wa BAKWATA Bukoba Vijijini na Maimam wa Misikiti, Katibu wa Mbunge Jason Lwankomezi amesema Futari hiyo itawafikia waamini wa Dini ya Kiislaam kupitia Misikiti iliyopo katika maeneo yao.

“Futari hii inawalenga waamini wote ambao wapo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni desturi yake yenye lengo la kuleta umoja, upendo na mshikamano katika jamii,” alisema.

Kwa upande wake Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Bukoba Vijijini, Ahmed Baitu amemshukuru kwa Futari hiyo na kumsihi Mbunge wa Jimbo hilo kuendelea kuikumbuka jamii yake katika kipindi chote.

Naye Imam wa Msikiti wa Katoma, Yakub Abdallah Bishazo amesema alichokifanya Dkt. Rweikiza ni ishara ya kujali, hivyo wanamuombea mema, huku Mwenyekiti wa Vijana BAKWATA Bukoba Vijijini, Shafi Abudkadri kwa niaba ya Vijana akitoa shukurani kwa Mbunge huyo.

Maamuzi ya Xavi yaipasua FC Barcelona
Wachochezi, waanzisha vurugu nina taarifa zenu - RC Mwasa