Benki kuu ya Zimbabwe, imeidhinisha sarafu mpya iliyoorodheshwa kwa bei ya dhahabu, ili kupambana na mfumuko wa bei nchini humo kufuatia mdororo wa uchumi kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Mkuu wa benki kuu ya taifa ya Zimbabwe, John Mushayavanhu amesema kuanzia leo April 6, 2024, Benki zitabadilisha pesa inayotumika sasa katika dola za Zimbabwe, kuwa sarafu mpya iitwayo Zimbabwe Gold, ZiG.

Taifa hilo, lina viwango vya juu zaidi vya mfumuko wa bei duniani, rasmi asilimia 55 ya mwezi Machi baada ya kufikia kiwango cha tarakimu tatu kwa mwaka 2023.

Dola ya Zimbabwe ilipoteza karibu asilimia 100 ya thamani yake dhidi ya dola ya Marekani katika mwaka uliopita, ikiuzwa kwa takriban dola 30,000 za Zimbabwe kwa dola moja ya Marekani, huku katika soko la magendo dola za Zimbabwe 40,000 ikiuzwa dola moja ya Marekani.

Usanifu darala la Bibi Titi - Mohoro kufanyika upya
Wanajeshi kuingia kati udhibiti wizi wa Mafuta