Zaidi ya watu 90 wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka kaskazini mwa nchi ya Msumbiji.
Wasafiri hao, walikumbwa na umauti Aprili 7, 2024 wakati wakikimbia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu wakitokea mji wa Lunga kuelekea Kisiwa cha pwani ya Nampula.
Vyombo vya Habari vya Msumbiji, vimeripoti kuwa Mashua hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukuwa watu 100, lakini wakati inazama ilikuwa imepakia watu wapatao 130.
Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), limearifu kuwa Msumbiji inakabiliwa na mlipuko wa kipindupindu ambao haujawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya robo karne.
UNICEF imeeleza kuwa tangu kuanza kwa mlipuko huo Septemba 2022, zaidi ya watu 37,000 wamesha ambukizwa.