Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ametoa maagizo kwa wataalamu wote wa ardhi nchini kuhakikisha wanafika katika maeneo ya wananchi kuwaskiliza pamoja na kutafuta kitabu maalumu (logbook), cha kuandika taarifa zao za kazi za kila siku zikiambatana na saini ya mwenyekiti wa sehemu husika atakapofanya kazi hizo.
Waziri Silaa ameyasema hayo wakati alipokutana na wataalamu wanaohusika na kuratibu mpango wa kiwanja Cha mama Samia kilichopo kata ya Olmonti huku akibainisha siku ambazo wataalamu hao wa ardhi wanatakiwa kufanya shughuli hizo na kuwahimiza watanzania wasio na hati za ardhi kuzichukua mara moja.
Naye Mbunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo amemuomba Waziri Silaa kuhakikisha wakati wa upimaji wa maeneo hayo hususani yatakayogusa ujenzi wa barabara kujumuisha watu wote katika umegaji wa ardhi ili kuepusha migogoro kwa wananchi.