Boniface Gideon – Tanga.

Miradi 8 yenye zaidi ya sh bilioni 11 inatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru jijini Tanga Aprili 14, ambapo utakimbizwa km 99.3, katika tarafa 4, kata 14 na mitaa 81 ya Wilaya hiyo.

Pia Mwenge huo utahamasisha shuhuli mbalimbali za Wananchi, ikiwemo Serikali za mitaa, lakini pia mapambano dhidi ya vvu, malaria, dawa za kuleya, rushwa pamoja na uhamasishaji wa lishe bora.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji akitoa taarifa ya mbio za Mwenge huo ofisini kwake, amesema mara baada ya mapokezi utakagua namna Halmashauri hiyo inavyotunza mazingira na kudibiti taka ngumu katika dampo la Mpirani na kupanda miti 50 ya matunda.

Amesema piabutafungua mradi wa maji mtaa wa Putuni wenye thamani ya takribani sh bilioni 2, lakini pia utakagua miti 300 iliyopandwa wakati wa mapokezi ya mwenge mwaka jana katika shule ya sekondari Kiomoni.

Hata hivyo Kaji ametoa wito kwa wakazi wote wa Wilaya ya Tanga kujitokeza kwa wingi katika mapokezi, katika njia utakapopita mwenge wa uhuru katima maeneo yavmiradi na eneo la mkesha.

“Mkesha utafanyika katika shule ya sekondari ya Usagara, tumeandaa burudani ya kutosha, Mwenge ni furaja, tunataka hilo lionekane kweli, baada ya shuhuli nzima ya mchana, ikifika jioni wote tukutane pale tufurahi na kukesha na mwenge wet wa uhuru,

Mafuriko: CCM Dar es Salaam waigusa jamii Rufiji
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 14, 2024