Mwanaume mmoja (40), ambaye aliwashambulia na kuwauwa watu sita kwenye duka moja mjini Sydney nchini Australia, na kuwajeruhi wengine kadhaa ameuawa.

Kamishna Msaidizi wa Polisi, Anthony Cooke  Amesema mshambuliaji huyo alifanya tukio hilo akiwa peke yake na hakukuwa na kitisho cha kuendelea kwa shambulizi hilo.

Naye Kamanda wa Polisi wa Sydney, Karen Webb amesema waliouawa ni wanawake watano na mwanamme mmoja na waliojeruhiwa ni wanane akiwemo mtoto mdogo wa miezi tisa.

Waziri Mkuu wa Australia, Antony Albanese amelaani shambulio hilo ambalo hadi sasa dhamira ya aliyelifanya haijafahamika, huku Mfalme Charles III wa Uingereza na mkewe Camilla wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliotuma salamu za rambirambi na pole.

DC Malisa aingilia kati mgogoro Soko la Wamachinga Old Airport
Mafuriko: CCM Dar es Salaam waigusa jamii Rufiji