Scolastica Msewa, Rufiji – Pwani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amepokea Msaada wa magari kumi kutoka jeshi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ, kwa ajili ya shughuli za kusafirisha chakula kwenda kwenye makambi ya Waathirika wa mafuriko ya mto Rufiji katika Wilaya za Rufiji na Kibiti.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kupokea magari hayo huko Ikwiriri Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, Kunenge alisema wamepata misaada ya vyakula lakini kulikuwa na changamoto ya usafiri kutokana na miundombinu kuharibiwa na mafuriko yanayoendelea.
Aidha, limshukuru Amiri jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa Majeshi General Mkunda kwa Msaada huo.
Maafisa 14 wa JWTZ miongoni mwao kuna mafundi na watasaidia kusambaza chakula kwa walengwa Waathirika wa mafuriko ya mto Rufiji.