Klabu ya Arsenal imeaanza mazungumzo na Gabriel Magalhaes kuhusu mkataba mpya na ulioboreshwa, kwà mujibu wa ripoti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ameekuwa PATNA mnzuri na William Saliba katika safu ya ulinzi ya Arsenal, na kuisaidia klabu hiyo kuuwinda ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo.
Washika Bunduki’ hao kwa sasa wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu mbele ya Manchester City kwa tofauti ya alama moja baada ya michezoya jana Jumapili (Aprili 28).
Liverpool pia wako kwenye kinyanganyiro hicho, lakini waliona matumaini yao yamefifia, baada ya sare ya 2-2 dhidi ya West Ham Utd, juzi Jumamosi (Aprili 27)
Gabriel tayari ana mkataba wa kuendelea kuitumikia Arsenal hadi 2027, lakini Evening Standard limeripoti kwamba mazungumzo yanaendelea na wawakilishi wa mchezaji huyo kuhusu suala la kuboreshwa kwa mkataba mpya.
Iwapo Gabriel atapata mkataba mpya, atafuata nyayo za Saliba, ambaye alitia saini mkataba mpya Julai mwaka jana akiweka mustakabali wake Arsenal hadi 2028, na Ben White, ambaye amepata uhakika mkubwa kutokana na kiwango chake cha beki wa kulia.
Mbrazil huyo amecheza mechi 46 katika mashindano yote msimu wa 2023/24, akiimarisha nafasi yake pamoja na Saliba, ambaye amefurahia kampeni ya kuvutia.
Aliwasili Septemba 2020 kutoka Lille kwa mkataba wa thamani ya Pauni milioni 27, na alisaini mkataba mpya wa miaka mitano na miwili baadae baada ya kuwa kiungo mkuu wa kikosi cha Arteta.
White aliweka mustakabali wake Arsenal kwa miaka mingine minne mwezi Machi, huku kiwango chake cha kuvutia kilisababisha wito wa Gareth Southgate kumrejesha kwenye kikosi cha England kwa mara ya kwanza tangu arejee nyumbani mapema kutoka Kombe la Dunia la 2022.