Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA, imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli nchini ambazo zimeanza kutumika hii leo Mei Mosi, 2024.

Taarifa ya EWURA imeeleza kuwa mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Mei 2024 yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 3.90 kwa mafuta ya petroli na kupungua kwa wastani wa asilimia 1.31 kwa mafuta ya dizeli

Bei za rejareja katika Mkoa wa Dar es Salaam ni petroli shilingi 3,314, Dizeli shilingi 3,196 na mafuta ya taa Tsh 2,840, Mkoa wa Tanga petroli shilingi 3,360, Dizeli shilingi 3,242 na mafuta ya taa shilingi 2,886 wakati Mtwara petroli shilingi 3,317, Dizeli shilingi 3,200 na mafuta ya taa shilingi 2,913.

Aidha, mabadiliko hayo pia yamechangiwa na kubadilika kwa kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni (exchange rate) na kuendelea kutumia euro kulipia mafuta yaliyoagizwa.

 

Hatujashindwa kusimamia usafirishaji - Mrisho
Lissu: Kutofautiana sio kosa la jinai