Serikali imeendelea kutoa tahadhari, huku ikiwataka Wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi wakati huu ambapo bado Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi wakati wa ziara ya kukagua baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na maafa ya mafuriko yaliyotokea Kata ya Msaranga, Mji Mpya na Kimochi Mkoani Kilimanjaro.

Amesema, “Serikali itaendelea kukabiliana na maafa mbalimbali nchini kwa kuendelea kutoa elimu juu ya namna ya kujiandaa na kukabili maafa ili kuondokana na madhara yatokanayo na maafa pindi yanapotokea.”

Aidha, Dkt. Yonaz pia amewataka Wananchi hao kuzingatia taarifa zinazotolewa na Serikali pamoja na kuendelea kuchukua tahadhari, ili kuendelea kuwa salama kipindi chote ambacho mvua hizo bado zinaendele kunyesha.

De Zerbi anukia FC Bayern Munich
Wojciech Szczęsny kurudi London