Klabu ya Newcastle United inapewa nafasi kubwa ya kumsajili Beki kutoka nchini England na Klabu ya Fulham Abdul-Nasir Oluwatosin Oluwadoyinsolami “Tosin” Adarabioyo.
Adarabioyo amekuwa gumzo katika kipindi hiki kufuatia kuonesha kiwango safi akiwa na Klabu yake ya Fulaham, ambayo hadi sasa imejihakikishia kuwa sehemu ya klabu 20 zitakazoshiriki Ligi Kuu ya England msimu ujao 2024/25.
Newcastle United inatajwa kuwa katika mpango wa usajili huo, wakizipiku klabu nyingine za England Tottenham na Manchester United huku AC Milan ya Italia ikitajwa kuwa kwenye vita hiyo.
Mkataba wa beki huyo mwenye umri wa miaka 26 unamalizika mwishoni mwa msimu huu, na tayari am eshathibitisha kutokuwa na mpango wa kuendelea kuitumikia Fulham.
Gazeti la The Sun limeripoti taarifa za Adarabioyo likieleza: “Newcastle wanakaribia kumsajili Beki wa Fulham Tosin Adarabioyo kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu 2023/24.
“Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameripotiwa kupewa ofa ya mkataba wa muda mrefu huko St James’ Park wenye thamani ya zaidi ya Pauni 100,000 kwa juma.
“Kinda huyo wa zamani wa Manchester City hivi majuzi alisisitiza hamu yake ya kuondoka Fulham msimu wa joto wakati mkataba wake utakapoisha, ambapo SunSport ilifichua mnamo Desemba.
“Vilabu vingi kutoka nyumbani na nje vimekuwa vikimtazama Tosin, ikiwa ni pamoja na Manchester United, Tottenham na AC Milan.”