Afisa Wanyamapori ea Halmshauri ya Wilaya ya Kigamboni, Luciana Bashaija amesema watu watano wameripotiwa kujeruhiwa na mamba katika wilaya hiyo na kuwataka Wananchi kuchukua tafadhali hasa wanapopita kwenye madimbwi ya maji na mito.
Bashaija aliyasema hayo Wilayani Kigamboni Mkoani Dar es Salaam wakati TAWA ikitoa elimu kwa Wananchi kuhusu uwepo wa wanyama wakali uliosababishwa na uharibifu wa mazingira.
Amesema, wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuchukua tafadhali kuhusu uwepo wa wanyama hao wakali Mamba na Viboko kwenye makazi ya watu, akidai waliletwa na maji ya mafuriko ya mito na vijito.
TAWA inaelimisha kuwa, mahali penye vitendo vya uharibifu wa mazingira ni vichocheo vya mabadiliko ya tabia nchi ikisababisha uwepo wa mvua nyingi zinazopelekea mafuriko.
Pia wanasema hali hiyo husababisha kiangazi kikavu kinachopelekea Wanyamapori kutoka eneo moja kwenda jingine ikiwemo kwenye makazi ya watu hasa yale yaliyokaribu na vyanzo vya maji.
Aidha, TAWA inaelekeza kuwa uvuvi haramu wa kutumia sumu pamoja na shughuli za kilimo pembezoni mwa mito pia ni chanzo cha Mamba na Viboko kulazimika kuyahama makazi yao ya asili na kukimbilia kwenye maficho yaliyo jirani na makazi ya watu.