Shambulio dhidi ya kituo kimoja cha afya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, limesababisha vifo vya raia wanane, hali ambayo imezua wasiwasi miongoni mwa jamii na watoa huduma za afya.

Tukio hilo limetokea jimbo la Kivu Kaskazini ambapo mashuhuda walisema lilitekelezwa na wanamgambo wa Allied Democratic Forces ADC, ambao awali waliahidi uaminifu kwa kundi la Islamic State – IS mapema mwaka 2019.

Kiongozi wa Jumuiya ya kiraia wa Beni, Omar Kalisia amesema, kati ya waliofariki dunia ni pamoja na Wagonjwa na Mhasibu katika kituo hicho cha Afya na kwamba Muuguzi mmoja hakuwepo wakati Yukio hilo likitekelezwa, na nyumba moja ilichomwa moto.

Tukio hilo linakuja kufuatia shambulio la Mei 3, 2024 kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika jimbo hilo na shambulio jingine la Mei 7, 2024 katika kijiji kimoja cha jimbo la jirani na Beni.

MAKALA: Ukiuheshimu utaratibu utakuheshimisha
Watano wajeruhiwa na Mamba Kigamboni, tahadhari yatolewa