Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewataka Viongozi wa Mkoa huo kuwa kitu kimoja na kuacha ubinafsi katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta maendeleo na kuvutia wawekezaji kwenye fursa mbalimbli zilizopo.
Sendiga ameyoa rai hiyo hii leo Mei 11, 2024 alipoongoza kikao cha Viongozi mbalimbali wa Mkoa kujadili fursa za uwezekaji zilizopo katika Mkoa wa Manyara, katika ukumbi wa Chuo kikuu huria cha Wilayani Babati, Manyara.
Aidha, amewataka Wakurugenzi wote kwenda kusimamia ipasavyo Halmaahauri zao, ili kuleta uwekezaji wenye tija na kukusanya mapato, hasa katika eneo la Kilimo.