Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Manyara, Ladslaus Mtui amewataka wamiliki wa ardhi Mkoani humo ambao bado hawajalipa kodi ya pango la ardhi kukamilisha malipo hayo kabla ya Juni 30 mwaka huu kabla hawajachukuwa za kisheria.
Akizungunza na Vyombo vya Habari Mtui amesema kodi hizo zinatakiwa kulipwa katikaofisi zote za ardhi zilizopo Halmashauri zote za mkoa wa Manyara.
Ofisi hizo zitatoa huduma mbalimbali za ardhi kama utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa aliyoyatoa hivi karibuni.