Spika wa Bunge la Kaunti ya Kilifi Nchini Kenya, Teddy Mwambire ameishutuhumu Serikali kwa ubaguzi dhidi ya waathiriwa wa mafuriko katika kutoa usaidizi.
Mwambire amesema Wakulima ambao mazao yao yalisombwa na mafuriko msimu uliopita hawakulipwa fidia kinyume na inavyofanyika kwa Wakulima wa maeneo mengine ya nchi.
Mafuriko nchini humo hivi karibuni yalipelekea Mamlaka ya Barabara kuu – KENHA, kutangaza kufungwa kwa muda Barabara ya Garsen – Witu – Lamu, kufuatia kuongezeka kwa kina cha maji kwenye eneo hilo.
Mafuriko hayo, pia yamesababishwa na mto Tana kuvunja kingo zake baada ya Mvua kubwa iliyonyesha, huku Wasafiri wakitumia Mashua kuvuka katika maeneo kadhaa kaunti hiyo.