Klabu ya Arsenal inatajwa kuongoza katika mbio za kumuwania Mshambuliaji kutoka nchini Brazil na Klabu ya Newcastle United Bruno Guimarães Rodriguez.

Guimarães amekuwa sehemu ya Washambuliaji wanaotajwa kuwa tishio katika Ligi Kuu ya England msimu huu, kufuatia kiwango kizuri alichokionesha na kuisaidia Newcastle United kufikia malengo yake.

Hata hivyo inaelezwa kuwa huenda Arsenal wakakabiliwa na upinzani kutoka kwa Mabingwa wa Soka nchini Hispania Real Madrid na Paris Saint-Germain ya Ufaransa, licha ya kuendelea kutajwa kama vinara wa kuifukuzia saini ya Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

“Arsenal wamewasiliana na Uongozi wa Bruno Guimaraes ili kufanikisha usajili wa Mshambuliaji huyo Newcastle,” gazeti la The Sun limeandika

“Kiwango kizuri cha Guimaraes kimemfanya avutiwe na pande kadhaa zikiwemo Real Madrid na Paris Saint-Germain. Lakini gwiji wa uhamisho Ben Jacobs anadai Arsenal wanaongoza mbio hizo.”

“Thomas Partey anaweza kuondoka msimu huu wa joto baada ya kuhangaika kuwa fiti. Mo Elneny pia anatarajiwa kuondoka baada ya Jorginho kukabidhiwa mkataba mpya wa mwaka mmoja.

“Na Arsenal sasa wanatazamia kumsajili Guimaraes ili kutengeneza pacha na Declan Rice. Wakati mkataba wa Guimaraes una kifungu cha kuuzwa kwa Pauni Milioni 100 na kitaanza kutumika mwezi wa Juni.

“Hata hivyo, ripoti inaongeza kuwa Newcastle itazingatia ofa za Pauni Milioni 80 na kuendelea kutoka kwenye klabu ambazo zimefuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.”

Udhibiti wa Ujangili: Rais Samia, Wananchi watajwa
Mbadala wa Erik Ten Hag atajwa