Klabu kadhaa za nchini Saudi Arabia zimeonyesha utayari wa kumuwania Kiungo kutoka nchini Brazil na Klabu ya Man Utd Carlos Henrique Casimiro, ambaye ni dhahir hatakuwa na nafasi kwenye kikosi cha miamba hiyo ya mjini Manchester msimu ujao.

Mashetani Wekundu wamekuwa na mwenendo mbaya hivi karibuni, wakishinda mchezo mmoja tu kati ya saba iliyopita ya Ligi Kuu ya England, huku Casemiro akishutumiwa na mashabiki kama kikwazo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ana nia ya kuondoka kwenda Saudi Pro League, lakini bado haijafahamika klabu ipi atakayoitumikia.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti hilo imeeleza: “Bado ana miaka miwili ya kuendelea na mkataba wa thamani ya £350,000 kwa wiki.

“Lakini Fabrizio Romano anadai Casemiro na United wakafikia makubaliano ya kuvunja mkataba uliopo baina yao, ili kutoa nafasi kwa mchezaji huyo kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

“Anafikiri vilabu vingi nchini Saudi Arabia vinatayarisha ofa za kumsajili nyota huyo kutoka Old Trafford.

“Wengi wamekuwa na Casemiro kwenye orodha yao ya walioteuliwa tangu Oktoba.

“Na mapendekezo yanatarajiwa kuwasilishwa mara tu bajeti ya ligi itakapoamuliwa na wakuu wa Saudia.

“Casemiro anaweza kuchukua nafasi ya kutimkia Mashariki ya Kati, na inaelezwa atalipwa mshahara mkubwa zaidi.

Bwanga, Mkola wamuibua Ibrah Class
Utekelezaji wa sheria: Ndejembi aipa somo OSHA