Beki wa Bayer Leverkusen na Uholanzi, Jeremie Frimpong, bado anataka kuendelea kusalia katika timu hiyo licha ya uwepo wa timu kibao kama Real Madrid, Manchester City, Arsenal na Manchester United zilizo tayari kuvunja mkataba wake kwa kutoa Pauni 35 milioni iliyoainishwa katika kipengele cha kuuvunja.
Frimpong mwenye umri wa miaka 23, inaelezwa anataka kubaki Leverkusen kwa msimu mmoja zaidi kabla ya kuamua kuondoka mwisho wa msimu ujao.
Awali beki huyu ilielezwa kutaka kujua hatma ya kocha wake Xabi Alonso kabla hajafanya uamuzi ikiwa atabaki ama ataondoka na baada ya kujiridhisha kocha huyo atabaki na yeye pia amemua kusalia walau kwa msimu mmoja.
Timu nyingi zimevutiwa na kiwango cha Leyerkusen alichokionyesha tangu kuanza kwa msimu huu kiasi cha kuisaidia klabu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Ujerumani.
Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 14.