Lydia Mollel – Morogoro.

Mahakama ya  Hakimu Mkazi Morogoro, imemuhukumu Mohamed Omary Salahange (38) kwenda jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wake wa  kike wa kufikia kwenye kesi namba 8112/2024 iliyokuwa ikimkabili.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, Renatus Barabara amesema Mahakama imemtia hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na ule wa utetezi.

 

Mahakama ilipokea vidhibiti na mashaidi sita upande wa Jamhuri, huku upande wa utetezi Mshtakiwa akijitetea mwenywewe bila Mwanasheria.

Licha ya ushaidi uliotolewa Mahakama inaamini kuwa muhanga wa tukio hilo alipoteza matumaini ya kuaminiwa pindi alipomueleza mama yake mzazi ambae sasa ni marehemu vitendo anavyotendewa na kudai kuwa anataka kugombanisha familia, hivyo mahakama kuridhika na ushaidi uliotolewa.

 

Akijitetea Mahakamani hapo, mshtakiwa aliieleza kesi hiyo ni yakutengeneza na kwamba yeye hahusiki hivyo anaiomba mahakama iamini hivyo.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi nne  ikiwemo ya mauaji ya mkewe Beatrice Talius Ngongolwa (38), kumuua kisha kumzika kwenye chumba walichokuwa wakiishi, kesi mbili za ukatili ambayo moja tayari amehukumiwa miaka 30 jela na nyingine  bado ipo Mahakamani.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 17, 2024
Morogoro: Aliyesabajisha vifo vya watu saba adakwa