Serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, ipo katika jitihada za kukamilisha mabadiliko ya sera ya Wazee ikiwemo umuhimu wa jamii kujiandaa kabla ya uzee, huduma wa afya ya akili na msaada wa kisaikolojia, miundombinu na mazingira wezeshi na uwezeshwaji wa wazee kwenye mabadiliko ya Teknolojia.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima Bungeni Jijini Dodoma, Wakati akisoma Makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2024-2025 na kusema Ustawi wa Wazee ni jambo lililopewa kipaumbele.

Amesema, “kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020- 2025 kwenye Ibara ya 91 ambayo imefafanua umuhimu wa kuimarisha utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii kwa wazee na ni jambo lililopewa kipaumbele. Kukosekana kwa fedha za utekelezaji wa Miradi ya Ukarabati wa Makazi ya Wazee kunaathiri utekelezaji wa ilani ya chama kwa kiasi kikubwa na hivyo kushindwa kuwapa Wazee Haki zao za Msingi.”

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa, “Kamati inaishauri Serikali kutoa fedha zilizotengwa kwaajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Ukarabati wa Makazi ya Wazee ili kuchochea Ustawi wa Wazee nchini na pia Serikali ione umuhimu wa kutoa fedha kwaa ajli ya kuweka nishati safi na salama ya kupikia katika makazi ya wazee.”

Hata hivyo, amesema kamati imebaini kuwa takwimu za miaka mitatu ya nyuma 2020/2021-2022/2023 Wizara imekusanya wastani wa asilimia 69 ya mapato iikilinganishwa na makadirio hivyo Wizara imepunguza makadirio ya mapato kwa mwaka 2024/2025 ili kuendana na uhalisia.

Ujio wa uchaguzi: TAKUKURU yautahadharisha umma
Haki Rasilimali wakamilisha utafiti mradi wa LNG