Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kutoka katika Vyombo mbalimbali vya Habari zinasema Rais wa Iran, Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian wamefariki dunia kwa ajali ya Helikopta.
Afisa Mkuu wa Iran ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, akihojiwa na Shirika la Habari la Reuters amesema Viongizi hao wawili, wanadaiwa kukumbwa na umauti baada ya Helikopta hiyo waliyokuwa wakisafiria kuanguka kwenye mlima kufuatia hali mbaya ya hewa na ukungu katika jimbo la Mashariki ya Azerbaijan.
Afisa huyo aliomba jina lake lisitajwe kutokana na unyeti wake Serikalini, na alinukuliwa akisema, “Rais Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje na abiria wote waliokuwemo kwenye Helikopta hiyo wamefariki katika ajali hiyo.”
Shirika la Habari la Iran la Mehr wakati huo huo nalo liliripoti kwamba abiria wote waliokuwemo walifariki na kwamba wengine waliokuwemo kwenye Helikopta ni pamoja na Gavana wa Azerbaijan Mashariki, Malek Rahmati.
Mwingine ni Ayatollah Mohammad Ali Ale-Hashem, ambayebl ni Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Mkoa wa Azarbaijan Mashariki.