Inaelezwa Uongozi wa Klabu ya Simba umetenga fedha za kutosha kwa ajili ya kufaniki sha usajili wa kiungo wa klabu ya Azam FC Feisal Salum ‘Fei Toto’ ili ajunge na timu hiyo.

Mbali na Fei Toto Simba SC pia inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Young Africans Stephane Aziz Ki katika haraka zao za kuimarisha na kurudisha heshima ya klabu hayo

Aziz Ki ni kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ambapo mpaka sasa ana mago 15 akifungana na Fei Toto hata hivyo mikataba wa mchezaji huyo ndani ya Young Africans unamalizika mwishoni mwa msimu huu

Mbali na Simba SC pia inaelezwa kuna timu kutoka Afrika Kusini ambazo zinafanya mchakato wa kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Burkina Faso

Akizungumza jijini Dar es salaam Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema klabu hiyo ipo makini katika usaliji na mchezaji wanayemtaka hawatashindwa kumsaji.

Amesema wanafahamu kiungo huyo mkataba wake unaenda ukingoni ingawa kwa Fei Toto mambo sio mepesi kutokana na nyota huyo kuwa na mkataba hai na Azam FC.

“Ni kweli hao wachezaji wawili wapo kwenye mipango yetu mmoja mkataba wake umefikia ukingoni na bado hajasaini mkataba mpya, kwa Fei Toto ni suala la kuweka fedha mezani ili kumchukua.” amesema Ahmed

“Pia kuna wachezaji wengine wapya tunawafuatilia sokoni kulingana na mapendekezo ya Benchi la Ufundi kwa ajili ya kuwasajili na kuimarisha kikosi chetu kuelekea msimu ujao” amengeza Ahmed

Amesema uongozi wa klabu hiyo utawasilisha ofa yao Azam FC kuangalia uwezekano wa kumchukua kiungo huyo wa timu ya taifa Taifa Stars na Zanzibar.

Rodri: Arsenal hawakuwa tayari kwa Ubingwa
Athari za Mafuriko: Mawaziri watatu matatani kwa uzembe