Nahodha na Kiungo wa Arsenal Martin Odegaard ana imani kuwa hivi karibuni kikosi chao kitapata mafaniko ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu, baada ya kutoka kappa msimu huu 2023/24.

The Gunners wamemaliza msimu kwa tofauti ya alama mbili chini ya Manchester City iliyotangaza Ubingwa wake wanne mfululizo jana Jumapili (Mei 19), kwakuifunga West Ham Utd 3-0, huku Arsenal ikiilaza Everton mabao 2-1.

Odegaard aliyesajiliwa Arsenal mwaka 2021 akitokea Real Madrid ya Hispania amesema: “Nina furaha tumepata ushindi, kumaliza na ushindi nyumbani ndicho kitu pekee tulichotaka kufanya. Tulifanya hivyo lakini kwa bahati mbaya hatukupata bahati iliyohitajika na tulikuwa karibu sana kutwaa Ubingwa msimu huu.

“Tumepiga hatua kubwa ukilinganisha na msimu uliopita, tulikuwa bora zaidi na tumekomaa zaidi na Rekodi mpya ya ushindi kwenye ligi, kwa hivyo tunafanya mambo mengi mazuri na ni suala la muda hadi tuchukue mataji makubwa. Tutaendelea kupambana kwa moyo wetu wote ili kufikia malengo ya kuwafurahisha mashabiki wa Arsenal duniani kote.

“Tunaruhusiwa kuhisi kukatishwa tamaa kidogo kwa sasa, tulikuwa karibu sana na Ubingwa. Lakini ukiangalia msimu, umekuwa wa kushangaza kwetu kwa sababu hatujafikia lengo. Nadhani hatua tunazochukua kote zinashinda nguvu zaidi kuliko mwaka jana.”

Ameongeza: “Ninajivunia kuwa sehemu ya wachezaji walioipambania Arsenal na ninajivunia timu hii.

“Sapoti ambayo tumekuwa nayo kwa msimu mzima ugenini na nyumbani kila mahali ilikuwa kubwa sana. Tunawapenda sana na tunatumai msimu ujao tunaweza kurejea na kuwapa Ubingwa mashabiki wetu na kusherehekea pamoja.”

Ummy: Wanawake, Vijana changamkieni fursa za kiuchumi
Dkt. Tax: Wizara kufanya tathmini hali ya mafunzo JKT