Wizara ya UIinzi na Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 limeendelea kuimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, mafunzo na mazoezi pamoja na rasiIimaIi watu, huku ikikusudia kufanya tathmini ya hali ilivyo ya mafunzo ya JKT na kuandaa Mpango Mkakati utakaoainisha mahitaji, bajeti na muda wa utekeIezaji, kwa lengo la kuwachukua vijana wote wanaostahiIi kupata mafunzo ya JKT kwa kundi la lazima.

Hayo yamesemwa hii leo Mei 20, 1024 Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Ulinzu na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax wakati akisoma hotuba ya Mpango na Mwelekeo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 wa wizara hiyo.

Amesema, Wizara imeendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi wa Jeshi ikiwemo masIahi, huduma bora za afya na makazi pamoja na Kuimarisha miundombinu mbaIimbaIi katika maeneo
ya Jeshi.

“ Vilevile Kuimarisha mashirika na taasisi katika Sekta ya Ulinzi, KuendeIea kushiriki katika ujenzi na uIinzi wa miradi ya kimkakati kwa masIahi mapana ya Taifa, KuendeIea kuimarisha uwezo wa Jeshi Ia Kujenga Taifa kwa kuboresha miundombinu iIi Iiweze kuchukua vijana wengi zaidi watakaopata mafunzo ya uzaIendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa, na stadi za kazi kwa vijana wa kundi la lazima na wakujitoIea,” amesema Tax.

“Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya za Kikanda, na nchi mbalimbali katika nyanja za kijeshi na kiuIinzi na hivyo kuimarisha Diplomasia ya Ulinzi, KuendelIea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kukabiliana na majanga na dharura inapohitajika,” amebainisha.

Aidha amesema kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, Shirika Ia Uzalishaji Mali la Jeshi Ia Kujenga Taifa (SUMAJKT), liliidhinishiwa jumla ya Shilingi 3,000,000,000.00 kwa ajili ya ununuzi wa zana za kilimo na kuongeza kuwa, “kiasi hiki cha fedha kimechangia katika kuimarisha uzalishaji wa chakuIa iIi kuipunguzia Serikali gharama za maIezi ya vijana wanaojiunga na mafunzo ya Jeshi Ia Kujenga Taifa na kuiwezesha JKT kujitosheleza kwa chakulIa kwa vijana wa JKT, na kuchangia pia katika usalama wa chakula na uzalishaji wa mbegu.”

Ameongezea “Katika kipindi cha kuanzia mwezi JuIai 2023 hadi Aprili 2024, SUMA JKT limeendeIea kutekeleza shughuli za uzalishaji mali kupitia kampuni tanzu na viwanda vyake, Shughuli hizo zinatekeIezwa kupitia sekta ya ujenzi, viwanda, biashara na huduma, kilimo, mifugo na uvuvi,” amesema Tax

Odegaard: Mafanikio ya ubingwa hayako mbali
Muheza wazindua kampeni kunusuru rasilimali za Bahari