Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, iliyopo The Hague nchini Uholanzi, imetoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa usalama, Yoav Gallant.

Hatio hiyo, imetolewa na ICC ikidai kuwa wawili hao wanahusika na uhalifu wa kivita pamoja na makosa ya uhalifu wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza.

Wakati hayo yakijiri, mapigano makali yameripotiwa katika kambi ya kati ya Nuseirat tangu jeshi lianzishe operesheni inayolenga mji wa kusini wa Rafah, huku Wanamgambo wa Kipalestina na Wanajeshi wa Israel pia wakipambana katika kambi ya Jabalia kaskazini mwa Gaza.

Katika mapigano hayo, shambulio la anga la Israel lililolenga nyumba moja katika kambi ya wakimbizi katikati mwa ardhi ya, Palestina liliua takriban watu 20, huku ikidaiwa waliojeruhiwa ni pamoja na watoto kadhaa, na waokoaji walikuwa wakitafuta watu waliopotea na walionaswa chini ya vifusi.

Pochettino afichua kukutana na bosi Chelsea
Mafuriko: Sillo awatembelea Wakazi waliokosa pa kuishi, chakula