Awamu ya kwanza ya mbegu zenye thamani ya shilingi 63,700,000 zimepokelewa Rufiji kutoka kwenye ya ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa kwa ajili ya kusaidia Wananchi ambao mazao yao yalisombwa na maji ya mafuriko ya mto Rufiji hivi karibuni.
Mbegu hizo, zimepokelewa katika ghala la Ikwiriri wilayani Rufiji ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Waziri Mchengerwa kutoka katika michango ya milioni 50 alizotoa yeye mwenyewe, Wakuu wa mikoa 26 nchini kutoa michango ya shillingi milioni 44 na shilingi milioni 13.7 kutoka kwa wazawa wa Rufiji wanaoishi nje ya Rufiji na kufanya Jumla ya shillingi milioni 107.7.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Gowele amesema alikabidhiwa na Waziri Mchengerwa fedha hizo hivyo manunuzi ya mbegu hizo ni sehemu ya fedha kiasi cha shilingi milioni 63.7 ambapo bado kuna Salio la mbegu zingine zenye thamani ya shilingi milioni 43 zitaletwa
Usambazaji wa Mbegu hizo kwa awamu ya kwanza umefanyika ambapo jumla ya kilo 8,984 za mbegu hizo zimesambazwa katika kata za Mwaseni, Kipugira na Ngorongo huku akitoa wito kwa taasisi na mashirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na Watu binafsi kuendelea kuunga Mkono juhudi za Serikali pamoja na Mbunge wa Jimbo Hilo kuwasaidia Mbegu wananchi hao Ili kurudisha Hali Kilimo kama ilivyokuwa awali.