Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri amezindua kampeni ya upandaji miti katika kata ya Miyuji Jijini Dodoma.

Uzinduzi huo umefanyika hii leo kwa upandaji miti ya Matunda 25, huku akiwataka Wakazi wa kata hiyo kuiga mfano bora kwa walioshiri zoezi hilo.

Amesema, “kwanza kabisa niwapongeze kata ya miyuji kwa kupanda miti hii ya matunda katika ofisi yetu ya kata, najua kupitia nyie viongozi ambao mmeshiriki katika upandaji miti hii Wananchi wenu wataiga mfano mzuri kutoka kwenu.”

“Nataarifa inaonyesha hapa kuna kaya kama 3,000 na kuendelea kwahiyo kila kaya wakipanda mti mmoja mmoja ni sawa na miti 36,000, kwaio tukijitahidi kupanda miti na kutunza miti hii tutapata faida katika kaya yetu,” aliongeza Shekimweri.

Aidha, Mkuu huyo wa Eilaya pia amehaidi kutoa shilingi milioni moja na nusu kwa kwa kata itakayo simamia ajenda ya “MTI WANGU, KWA UCHUMI WANGU NA AFYA YANGU”.

“Na kwa wale ambao wamepanda miti leo wekeni vibao vya majina yenu katika kila mti, ili iwe kumbukumbu nzuri katika ofisi ya kata na Wilaya ya Dodoma kwa ujumla,” amesisitiza Shekimweri.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 26, 2024
Shirima: Gari la Zimamoto halifiki eneo la tukio bila Maji