Serikali Nchini, imesema gharama ya Shilingi 177,000 ya kuunganisha umeme Vijijini kwa Shirika la Umeme – TANESCO, ilifutwa na sasa huduma hiyo inatolewa kwa Shilingi 27,000.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahya Massare aliyetaka kujua ni lini serikali itarejesha gharama za kuungaishiwa umeme kuwa Shilingi 177,000.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Kapinga amesema, “kulingana na bei za umeme zilizopitishwa na EWURA, gharama za kuunganisha umeme wa njia moja katika maeneo ya vijijini ni Sh 27,000 na mijini Sh 320,960. Kwa kipindi cha nyuma, kwa miradi ya vijijini, REA ilikua inatoza Sh 27,000 na TANESCO Sh 177,000.”

Amesema, “kutokana na malalamiko ya wananchi ya utofauti wa bei kati ya REA na TANESCO ya kuunganisha umeme vijijini, Serikali iliamuru TANESCO kushusha bei ya kuunganisha umeme vijijini na kuwa Sh 27,000 kama REA na tofauti ililipwa na Serikali kama ruzuku kwa TANESCO.”

Mkataba TANESCO, SONGAS: Maslahi ya Taifa kuwekwa mbele
Aziz Ki: Nina ndoto za ubingwa wa Afrika