Mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Shirika la Umeme nchini – TANESCO na SONGAS utafikia ukomo Julai 31 mwaka huu, na tayari timu ya wataalam (Government Negociation Team – GNT) iliyoanza majadiliano mwezi Aprili, 2023 inatarajia kukamilisha majadiliano hayo kabla ya mkataba kuisha.

Hayo yamesemwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge Jesca Kishoa aliyetaka kujua makubaliano ya mkataba ujao kati ya SONGAS na Serikali yamefikia hatua gani ikiwa mkataba wa awali upo katika mwaka wa mwisho.

Naibu Waziri Kapinga amesema, Serikali itahakikisha maslahi ya Taifa yanazingatiwa kabla ya makubaliano yatakayofuata.

Mzize awajibu mashabiki wanaombeza
Kapinga: Kuunganisha Umeme ni Sh. 27,000