Viongozi wa vyama vya upinzani Nchini, wametakiwa kuacha tabia ya kupinga kila kitu kinachofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi, kwani imekuwa ikitekeleza shughuli za kimaendeleo bila ubaguzi.
Rai hiyo, imetolewa na Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei katika moja ya mahojiano ambayo amewahi kufanya katika studio za Dar24 Media zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam akisema suala hilo linarudisha nyuma nguvu kazi ya Taifa.
Amesema, “kuwa mpinzani haimaanishi kupinga kila jambo hata kama ni jema na kwa kufanya hivyo unakuwa huikomoi Serikali zaidi unawakosesha wananchi mambo ya msingi ikiwemo maendeleo.
“Vyama vya upinzani vinatakiwa kujadili hoja, na sio tu kujadili namna ya kumtoa kiongozi aliyepo madarakani na pia kizuri wakipokee maana Serikali haibagui na ndiyo dhana ya CCM, kuna majimbo mengine yameendelea vizuri licha ya kuwa yanaongozwa na upinzani,” aliongeza Dkt Kimei.