Wanafunzi waliokidhi vigezo wa shule za Serikali, zisizo za Serikali na watahiniwa wa kujitegemea ambao walifanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wapatao 188,787 wakiwemo wenye mahitaji maalum wapatao 812, wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati nchini kwa mwaka 2024 .
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa kuzungumzia uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi, uliofanyika kwa kuzingatia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.

Amesema, “wote 188,787, waliokidhi vigezo wakiwemo wenye Mahitaji Maalum 812 wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati katika fani mbalimbali. Wanafunzi 131,986 wakiwemo Wasichana 66,432 na Wavulana 65,554 wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano 622 zikiwemo shule mpya 82 zinazoanza mwaka huu.”
Mchengerwa ameongeza kuwa, Wanafunzi hao,  1,462 wakiwemo wasichana 669 na wavulana 793 wamepangwa katika shule za sekondari 8 zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi ambazo ni Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.
“Wanafunzi 6,576 wakiwemo wasichana 3,449 na wavulana 3,127 wamepangwa katika Shule za Sekondari za Kutwa za Kidato cha Tano,
Alisema pia wanafunzi 123,948 wakiwemo wasichana 62,636 na wavulana 61,312 wamepangiwa katika shule za Sekondari za Bweni za Kitaifa za Kidato cha Tano,” amesema Mchengerwa.
A ameongeza kuwa, Wanafunzi 56,801 wakiwemo wasichana 17,332 na wavulana 39,469 wamepangiwa kujiunga kwenye kozi na fani mbalimbali za Stashahada katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Mfuko wa Barabara wakusanya mapato kwa asilimia 77
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 31, 2024